SHABIKI WA SIMBA AMEITWA NA POLISI...MKASA MZIMA UPO HIVI A-Z
Habari za michezo

SHABIKI WA SIMBA ATOLEWA POLISI NA SHABIKI WA YANGA…AKABILIWA NA TUHUMA UCHOCHEZI

Marce Ben Komba April 21, 2024 8:52 pm

Mwanachama wa Klabu ya Simba maarufu kama GB64 hii leo ameachiwa kwa dhamana baada ya kushikiliwa na Polisi kabla ya mchezo wa watani wa jadi kwa kile kilichoelezwa kutoa kauli za uchochezi.

Mwanachama wa Klabu ya Young Africans maarufu Mwalimu Yanga ndie amemwekea dhamana mchana wa leo na pia kumkabidhi kiasi cha pesa Tsh 100,000 iliyochangwa na wadau wengine.

GB64 amekabidhiwa pia simujanja (smartphones) mbili na mashabiki hao ambazo aliwahi kuomba achangiwe ili aachane na matumizi ya kiswaswadu (simu kitochi).
Hongera Mwalimu Yanga kwa hili, Mpira sio uadui.

BENCHIKA KUSTAAFU SIMBA?…HAKUBALI KUHARIBU CV YAKE…TIMU ALIYOPITA ALISTAAFU FEISAL SALUM FEI TOTO AMPIGA KO AZIZ KI…VITA YA WABABE HAO YAPAMBA MOTO