Home Azam FC BAADA YA KUONA WABONGO WENGI NI ‘MIYEYUSHO’ AZAM WAMVUTA MMAREKANI KUWA BOSI...

BAADA YA KUONA WABONGO WENGI NI ‘MIYEYUSHO’ AZAM WAMVUTA MMAREKANI KUWA BOSI WAO…

 


Aliyekuwa kuwa Kocha msaidizi wa Columbus Crew, Abdihamid Moalin ameingia mkataba wa miaka miwili na Azam FC kuwa Mkurugenzi wa Ufundi wa Kituo cha Kukuza Vipaji maarufu kama Azam FC Academy. 

Moallin ambaye ni Mmarekani mwenye asili ya Somalia, alisaini mkataba mbele ya Afisa Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdulkarim.

Kocha huyo aliyewahi kuifundisha Horseed ya Somalia, pia atakuwa akifanya uchambuzi wa mechi za timu kubwa ya Azam FC.

Pia amewahi kufanya kazi kwenye Ligi Kuu ya Soka Marekani (MLS), katika timu ya Columbus Crew (2014-2016), kama Kocha Msaidizi wa timu hiyo na timu za vijana chini ya miaka 18 na 23 ikiwemo D.C United.

SOMA NA HII  ROBERTINHO AFUNGUKA HAYA KUHUSU LUIS MIQUISSONE