NYOTA wa Wydad Casablanca, Simon Msuva amesema wala hana presha ya timu ambazo wanaweza kupangwa nazo kwenye hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambayo inatarajiwa kuanza kutimua vumbi kuanzia Februari, mwakani.
Droo ya hatua ya makundi ya michuano ya kimataifa ambayo kwa Tanzania wawakilishi wake ni Simba upande wa Shirikisho, inatarajiwa kufanyika mwezi huu au Januari mwakani katika makao makuu wa Shirikisho la Soka Afrika (Caf), Cairo nchini Misri.
Msuva alisema timu yao ipo tayari kukabiliana na timu yoyote katika hatua hiyo ya makundi akiamini kuwa kuwa klabu kubwa au bingwa unapaswa kuonyesha ubora dhidi ya timu ngumu.
“Unapozungumzia vigogo wa Afrika, Wydad ni miongoni mwao. Kwa hiyo hatuna sababu ya kutufanya kuwa na hofu juu ya kukutana na timu yoyote. Sisi ni askari ambao tupo tayari kwa vita muda wowote haijalishi adui yetu ni wa namna gani,” alisema Msuva.
Msuva amekuwa na mchango mkubwa kwa Wydad Casablanca katika mchakato wa kupigania nafasi ya kutinga makundi, mshambuliaji huyo wa Kitanzania aliipachikia timu hiyo mabao mawili kwenye michezo miwili ya raundi ya pili.
Kwa ujumla msimu huu wa 2021/22, Msuva amehusika kwenye mabao tisa ndani ya michezo 13 ya mashi ndano yote ambayo ameic ezea Wydad Casablanca wenye jukumu zito la kutetea ubingwa wao wa ligi, ametupia kambani mabao sita na kutoa asisti tatu.
Ikiwemo timu ya Msuva anayoichezea huko Morocco, zifuatazo ni timu 16 zilizotinga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, wakiwemo wababe wa Simba, Jwaneng Galaxy.
Timu hizo ni Al Ahly na Zamalek (Misri), Al Hilal na Al Merrikh (Sudan), Mamelodi Sundowns na AmaZulu (Afrika Kusini), CR Belouizdad na ES Setif (Algeria), Esperance na Etoile du Sahel (Tunisia), Horoya (Guinea), Jwaneng Galaxy (Botswana), Petro Atletico na Sagrada Esperanca (Angola), Raja na Wydad (Morocco).
[…] Simba wakabie juu, kuwanyima pumzi mabeki wao. Angalizo kwa Simba ni kwamba, wachezaji wengi wa Wydad ni wazoefu lakini umri umeenda kidogo lakini haimaanishi hawana […]