news

KISA KIWANGO CHAKE…MAKAMBO ALIAMSHA YANGA…ATOA KAULI MOJA TU YA ‘HAPANA’

admin December 19, 2021 12:34 pm


HERITIER Makambo, nyota wa kikosi cha Yanga, ameweka wazi kuwa ukurasa wake wa mabao ndiyo kwanza unaanza kufunguliwa kwani hajachuja katika suala la ufungaji, akitamba kwamba akipewa nafasi atafunga.

Nyota huyo kwa sasa ni kinara wa utupiaji ndani ya Yanga kwenye Kombe la Shirikisho akiwa ametupia mabao matatu, ilikuwa mbele ya Ihefu FC wakati Yanga iliposhinda mabao 4-0.

Akizungumza na Championi Jumamosi, mshambuliaji huyo ambaye anapewa nafasi ya kuanza kesho mbele ya Tanzania Prisons kutokana na Fiston Mayele kuumia, alisema kuwa kazi bado inaendelea.

“Naona wanasema kwamba uwezo unakuwa umeshuka kwa kuwa sifungi, katika hilo ninasema hapana kwa sababu ili ufunge inabidi uwe unapata nafasi na pia nimekuwa nikifanya mazoezi kila siku jambo ambalo linalinda uwezo wangu.

“Ninachoweza kusema ni kwamba wasubiri, kazi bado inaendelea na kwa namna ambavyo mashabiki wamekuwapamoja nasi kila muda waendelee na moyo huo, sisi tutazidi kupambana kwa ajili ya kupata matokeo,” alisema Makambo.

KUHUSU ISHU YA WAWA KUTEMWA AU AACHWE…PAWASA AIBUKA NA HILI..ATOA ONYO KALI… KUHUSU ‘SURE BOY’ KUMALIZANA NA YANGA..BABA’KE ASHINDWA KUJIZUA..AFUNGUKA HAYA…ATAJA MGOGORO..

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply