Home Azam FC BAADA YA KUTOKA SARE NA MBEYA CITY…MAKOCHA WAPYA AZAM WAVUNJA UKIMYA…WATAJA MABADILIKO…

BAADA YA KUTOKA SARE NA MBEYA CITY…MAKOCHA WAPYA AZAM WAVUNJA UKIMYA…WATAJA MABADILIKO…


KAIMU kocha msaidizi mpya wa Azam, Mohamed Badru ameweka wazi kuwa benchi lao la ufundi linahitaji muda zaidi ili kusuka kikosi kitakachokuwa na mwendelezo wa matokeo mazuri ya ushindi.

Azam Jumatatu iliyopita walitangaza rasmi kuachana na aliyekuwa kocha wao Mzambia, George Lwandamina ambaye aliuandikia barua Uongozi wa klabu hiyo akiomba kujiuzulu na nafasi hiyo kuchukuliwa na mkurugenzi wa ufundi, Abdihamid Moalin huku Mohamed Badru akikaimu nafasi ya kocha msaidizi.

Badru juzi Jumamosi alikuwa sehemu ya benchi la ufundi la Azam lililoiongoza klabu hiyo kwenye mchezo dhidi ya Mbeya City ulioisha kwa sare ya mabao 2-2.

Akizungumza na Championi Jumatatu, kocha msaidizi wa Azam, Mohammed Badru alisema: “Tunashukuru kwa matokeo ya sare ambayo tuliyapata kwenye mchezo wetu uliopita dhidi ya Mbeya City licha ya kwamba haukuwa mpango wetu.

“Licha ya kwamba hatukupata ushindi, lakini tunajivunia mabadiliko makubwa ambayo kikosi kimeyaonyesha mpaka sasa, tunaamini tukipata muda zaidi wa kuwa pamoja basi tutarejesha ari yetu ya ushindi.”

SOMA NA HII  BAADA YA KUACHANA NA SIMBA...WAARABU WAMPA DILI LA 'CHAP CHAP' ZORAN MAKI...MSHAHARA WAKE MPYA BALAA TUPU...