news

MORRISON ‘BANA’…WAKATI WENZAKE WAKIENDELA KUPAMBANA ..YEYE YUKO KWAO AKIFANYA ‘PATI’…

admin December 24, 2021 1:00 pm

 


WAKATI Simba ikiwa mkoani Tabora tangu jana ikijifua tayari kuwavaa KMC leo kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Ally Hassan Mwinyi, winga wake Benard Morrison jana alikuwa na jambo lake.

Mchezaji Bora wa Simba kwa mwezi uliopita, yupo kwao Ghana kwa mapumziko maalumu na jana alikuwa na jambo lake la kurudisha shukrani kwa kutoa msaada kwa watu wenye uhitaji.

Taarifa kutoka Ghana zinasema, Morrison akishirikiana na faimilia yake waliandaa jambo hilo na kuliita ‘BM3fFamily Soccer Fest’, huku likifanyika kwenye viwanja vya Effia Police Park.

Vyakula, mavazi, vifaa vya michezo na mahitaji mengine ya muhimu katika jamii hiyo vilitolewa na Morrison ambaye amekuwa mhimili wa ndani ya Simba kwa msimu huu, akiisaidia kwenye mechi za ligi na zile za Kombe la Shirikisho Afrika.

PAMOJA NA KUKABIDHIWA RUNGU LA USAJILI..NABI AVUNJA UKIMYA..ATUPA KOMBORA KWA UONGOZI… WAKATI YANGA WAKIENDELEA KUTAKATAKA…NABI ALIA NA  ‘KAZI CHAFU’ WANAZOFANYIWA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply