News

KIMEUMANA HUKO..HITIMANA AVUNJA UKIMYA…AFUNGUKA A-Z SABABU ZA KUIKIMBIA SIMBA..ATAJA MKATABA..

admin December 30, 2021 10:56 am

 


BAADA ya Klabu ya Simba kutangaza kufikia muafaka wa pande mbili kuvunja mkataba wa kocha msaidizi wa timu hiyo, Hitimana Thierry, mwenyewe ameibuka na kufunguka sababu kubwa ya kuondoka kikosini hapo.

Juzi Jumanne, Simba ilitoa taarifa hiyo ikiwa ni takribani miezi mitatu imepita tangu Hitimana raia wa Burundi kujiunga na Simba Septemba, mwaka huu.

Akizungumza na Soka la Bongo, Hitimana alisema sababu kubwa ya yeye kuondoka Simba ni baada ya waajiri wake hao kushindwa kutimiza baadhi ya makubaliano waliyoingia wakati anasaini mkataba.

“Kumekuwa na taarifa nyingi zinazohusishwa na uamuzi wa mimi kuondoka Simba, lakini ukweli ni kwamba nimeachana na Simba kutokana na mambo mbalimbali.

“Kubwa zaidi ni kutotimiziwa yale ambayo yalikuwepo kwenye makubaliano wakati ninaingia nao mkataba, hivyo nikaona ni jambo bora kufikia muafaka wa pamoja tuachane salama.”

KUDADEKI….HII NDIO YANGA YA GSM…WACHEZAJI WAFANYIWA ‘KUFRU’ YA FUNGA MWAKA..SIMBA CHA MTOTO…. RASMI…AJIB MALI YA AZAM FC…SIMBA WAVUNJA UKIMYA..WAANIKA SABABU ZA KUMTEMA….

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply