news

KUDADEKI….HII NDIO YANGA YA GSM…WACHEZAJI WAFANYIWA ‘KUFRU’ YA FUNGA MWAKA..SIMBA CHA MTOTO….

admin December 30, 2021 10:52 am


WADHAMINI wa Yanga ambao ni GSM, wamewafanyia kufuru mastaa wa timu hiyo kwa kuwapatia vocha yenye thamani ya Sh milioni moja kila mchezaji iliyotumika kufanya shopping katika maduka yote ya GSM Group Limited.

Hiyo ikiwa ni siku chache tangu Yanga itoke kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Biashara United katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa wikiendi iliyopita kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar.

Mmoja wa wachezaji wa Yanga, amesema kuwa: “Katika kusherehekea Sikukuu za Krismasi na Mwaka Mpya, wachezaji wote tumepewa vocha yenye thamani ya shilingi milioni moja itakayotumika kufanya shopping katika maduka ya GSM.


“Wachezaji wote jana (juzi) tulifika Msasani Mall kwa ajili ya kuchukua mahitaji ikiwemo nguo, viatu na vitu vingine vyenye thamani hiyo.”

Nahodha wa Yanga, Bakari Mwamnyeto, alitumia ukurasa wake wa Instagram kuandika ujumbe wa kumshukuru bosi wa GSM ulisomeka hivi: “Shukran Boss GSM kwa zawadi ya leo (jana). Tunashukuru kwa ulichotupa dukani na sisi tutakupa uwanjani, kila hatua dua. Mungu wetu sote.”

KUELEKEA MECHI NA AZAM FC…PABLO HATAKI MZAHA… AFANYA MAAMUZI MAZITO SIMBA.. KIMEUMANA HUKO..HITIMANA AVUNJA UKIMYA…AFUNGUKA A-Z SABABU ZA KUIKIMBIA SIMBA..ATAJA MKATABA..

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply