Home news KIWANGO CHA LUIS MUQUISSONE CHAWALIZA MASHABIKI AL AHLY…WADAI NI HASARA KWA TIMU…

KIWANGO CHA LUIS MUQUISSONE CHAWALIZA MASHABIKI AL AHLY…WADAI NI HASARA KWA TIMU…


Licha ya Pitso Mosimane kuwapa Al Ahly taji la CAF Super Cup bado mashabiki wameendelea kumkosoa hasa baada ya Al Ahly kutoa sare ya 1-1 kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Future Fc.

Mashabiki wanakosoa selection ya Kikosi kwa kuanza na Kiungo Luis Miquissone mbele ya Taher Mohamed Taher na Hussein El Shahat ambao wao wanaamini kiwango cha Luis Miquissone kinaingia zaidi ya mara milioni kwa viungo hao.

Mashabiki wanaenda mbali zaidi na kusema mpango wa kumnunua Miquissone ni uharibifu wa pesa na wana muona kama dhaifu sana.

Hata hivyo baadhi yao wamekuwa na mawazo tofauti… wengine wanamkosoa Pitso kwa kumuingiza Rami Rabia

Al Ahly wameendelea kukaa juu ya msimamo wa ligi kuu nchini Misri wakiwa na alama 19 sawa na Zamalek aliepo nafasi ya pili ila Ahly ana faida ya mchezo mmoja mkononi.

Katika mechi 7 walizocheza msimu huu,Pitso amewaongoza Al Ahly kushinda michezo 6,sare 1 na hajapoteza.

SOMA NA HII  KAZE : TULITUMIA NGUVU KUBWA SANA KWENYE MECHI DHIDI YA SIMBA...