Home news BAADA YA AJIB KUTUA AZAM…MORRISON NAYE AITAKA AZAM FC…AM’BEMBELEZA PABLO KWA SIMU…

BAADA YA AJIB KUTUA AZAM…MORRISON NAYE AITAKA AZAM FC…AM’BEMBELEZA PABLO KWA SIMU…

 

UNAAMBIWA pamoja na Kiungo Mshambuliaji wa Simba raia wa Ghana, Bernard Morrison kukosekana kwa muda ndani ya timu hiyo akiwa ameenda kwao, lakini bado ametuma ujumbe kwa kocha wa timu hiyo, Pablo Franco akiomba awepo kwenye kikosi kitakachocheza dhidi ya Azam FC, wikiendi hii.

Morrison alitarajiwa kutua nchini mapema juzi Jumatano tayari kwa kuungana na wenzake kujiandaa na mchezo huo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa Uwanja wa Mkapa, Dar.

Chanzo chetu kutoka Simba, kimeliambia Spoti Xtra kuwa: “Kiukweli Morrison ana mapungufu yake ila linapokuja suala la kupigania namba, hajawahi kurudi nyuma.

“Licha ya kuwa safarini kwa muda, bado amekuwa akiwasiliana na kocha wetu, akimuomba sana hata kama ataingia nchini akiwa amechelewa basi ampatie nafasi ya kucheza dhidi ya Azam FC.

“Morrison ametua  tayari kwa kuungana na wenzake, ila pamoja na hilo anashauku kubwa sana ya kuonesha jambo katika mchezo huo.”

SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI YA KESHO NA WANIGERIA....NABI AANIKA MAMBO ALIYOYAONA KWA YANGA SC..