Home news BAADA YA KUISHUHUDIA SIMBA IKIIUA KMC..PABLO ATIKISA KICHWA ..ASISITIZA MAMBO BADO..

BAADA YA KUISHUHUDIA SIMBA IKIIUA KMC..PABLO ATIKISA KICHWA ..ASISITIZA MAMBO BADO..


KIKOSI cha Simba kimerejea jijini Dar er Salaam jana na wachezaji wake kupewa mapumziko mafupi kabla ya kurejea tena keshokutwa kuanza mazoezi ya kujiwinda dhidi ya Azam, huku Kocha Mkuu wake, Pablo Franco akisema utamu Msimbazi ndo sasa umeanza.

Kocha huyo alisema kurejea kwa nyota wake waliokuwa majeruhi kumempa faraja kubwa ya kuamini timu yakle itakuwa inatoa dozi za maana kwa wapinzani wao, tofauti na walivyoanza msimu walipokuwa wakipata ushindi kwa kuutolea jasho.

Simba juzi ikiwa ugenini mjini Tabora iliifumua KMC kwa mabao 4-1 ikiwa ni ushindi wao wa kwanza mnono, wakifuata nyazo za Azam, FC iliyotoa dozi kama hiyo siku moja kabla kwa Ruvu Shooting katika mfululizo wa mechi za Ligi Kuu Bara, pambano lililochezwa Azam Complex.

Pablo alisema kuimarika kwa eneo lao la ushambuliaji ndio furaha yake kwani ana uhakika wa kikosi chake kupata mabao mengi zaidi yatakayowasaidia mbele ya safari wakati ligi ikichangamka na hata kwenye michuano ya ASFC na Kombe la Shirikisho Afrika.

Kauli ya Pablo imekuja baada Chriss Mugalu na Pape Ousmane Sakho wakirejea uwanjani baada ya kukosekana kwa michezo kadhaa.

Kabla ya mechi ya juzi dhidi ya KMC, Simba ilikuwa imecheza mechi nane na kufunga mabao nane, kati ya hayo manne yakifungwa kupitia viungo wake Peter Banda, Mzamiru Yassin, Kibu Denis na Rally Bwalya na yaliyosalia yakiwa ya mshambuliaji wake hatari, Meddie Kagere.

Kwenye mechi ya juzi mabao mawili yalifungwa na Kibu Denis na mengine ya mabeki, Joash Onyango na Mohammed Hussein ‘Tshabalala’.

“Tumezidi kuimarika eneo la ushambuliaji baada ya Mugalu kurejea, pia kuna Sakho na tunaamini wakishirikiana na waliopo mambo yatakuwa mazuri zaidi, bado tuna safari ndefu katika msimu huu, tunahitaji kuwa bora na kufunga mabao mengi,” alisema Pablo ambaye kesho anatarajiwa kukutana na mabosi wake kwa ajili a kujadiliana kwa kina juu ya usajili kupitia dirisha dogo lililo wazi kwa sasa.

Mabosi wa Simba mezani kwao kuna majina matatu kati ya wanne inayowapigia hesabu likiwamo la Alex Bazo kutoka Nkana ya Zambia, Clatous Chama kutoka RS Berkane na Mkenya Harrison Mwendwa, huku jina lingine ambalo bado limefichwa likiwa la mzawa.

SOMA NA HII  BAADA YA KUMRUDISHA KISINDA NYUMBANI....YANGA HAWAJALAZA DAMU AISEE...WAMPA KAZI HII KUBWA YA KUFANYA...

Habari za ndani zilizothibitishwa na mmoja wa vigogo wa klabu hiyo ni kwamba, wamepanga kufanya kikao maalumu pamoja na Kocha Pablo, kesho Jumatatu ijayo ili kujadiliana juu ya usajili wa nyota wapya wanaotakiwa kusajiliwa kwenye dirisha hili.

“Tunasubiri timu irejee kutoka Tabora tutakaa pamoja ili kuwekana sawa na kupitisha wanaofaa kusajiliwa. Tunafanya hivi ili kuepuka lawama kama ilivyotokea baada ya tuliosajiliwa kwa sauti ya mtu mmoja, kushindwa kuwapa matokeo chanja,” alisema kigogo huyo.