Home news KISA BARBARA….YANGA WALIA NA KAULI TATA ZA BOSI WA SIMBA…WALIAMSHA KUTAKA UCHUNGUZI...

KISA BARBARA….YANGA WALIA NA KAULI TATA ZA BOSI WA SIMBA…WALIAMSHA KUTAKA UCHUNGUZI ‘FASTA’…


Uongozi wa Klabu ya Yanga umesikitishwa na kauli iliyotolewa na Mwenyekiti wa Wanachama wa Klabu ya Simba, Murtaza Mangungu , baada ya mchezo nambari 64 wa Ligi Kuu baina ya Simba na Yanga uliochezwa na Jumamosi tarehe Jumamosi ya tarehe 11/12,2021.

Kupitia vyombo vya Habari Ndugu Murtaza Mangungu aliishutumu Klabu ya Yanga kwa kuwaona watu wakiingia katika eneo la VVIP bila kuwa na kadi Mtendaji Mku wa Simba akizuiwa, na alitoa shutuma kwamba TFF kuwa na dhumuni la kuipa ubingwa Klabu ya Yanga msimu wa 2021/2021.

Kauli hizo na shutuma hizo si za kiungwana na zimechafua taswira ya Klabu na imeleta sintofahamu kubwa kwa wanachama , wanamichezo , wadhamini na wadau mbalimbali.

Klabu ya Yanga imesema haihusiki kabisa na utaratibu wa kuingia uwanjani kwa wageni wa VVIP, hivyo ineshangazwa na shutuma zilizotolewa na Mangungu kwani wao kama wageni wa mchezo walipatiowa kadi 30, VVIP zikiwa 20 ma VIP zikiwa 1o, hivyo kauli ya kusema kuwa watu wa Yanga wameonekana wamepita bila kuwa na tiketi au kadi ni kutaka kuonyesha kuwa wananchi hawafuati utaratibu na inapata upendeleo kutoka TFF kitu ambacho siyo sahihi na kinapeleka ujumbe mbaya kwenye jamii.

Pia Kiongozi mkubwa wa Klabu anapotoa shutuma nzito kwa Klabu ya Yanga kuwa imeandaliwa kupewa Ubingwa msimu huu , ni kutaka kuiaminisha jamii kwamba kuna mkakati wa upangaji wa matokeo baina ya TFF na Klabu ya Yanga, hizi ni tuhuma nzito ambazo zinahitajika kufanyiw auchunguzi wa haraka na mamlaka husika kuhakikisha uthibitisho unapatikana na hatua kali kuchukuliwa.

Mbali na kauli hizi za kusikitisha kwa wadau na wapenda mpira nchini, Yanga inapenda kuusia washirika wa ligi kuu ya NBC kuishi falsafa ya Mpira Play Fair, Be Positive na kutum,ia mchezo huu kuineemesha jamii.

Yanga kama Klabu ina dhima ya kuwa mfano bora katika jamii na itaendelea kuhamasisha katika ushindanio wa kiungwana na uwajibikaji, matokeo chanya jayawezi kuja kama hakuna uwekezaji na mahusiano mazuri baina ya klabu na wadau mbalimbali waliopo.

SOMA NA HII  HUKO YANGA MORRISON AZIDI KUFANYA MAAJABU....KWA MARA NYINGINE TENA JINA LAKE LATAJWA NA NABI...