Home Azam FC SAA CHACHE BAADA YA ‘KUTUMBULIWA’ AZAM FC…LWANDAMINA AANIKA HILI ..’AUVAMIA’ UONGOZI…

SAA CHACHE BAADA YA ‘KUTUMBULIWA’ AZAM FC…LWANDAMINA AANIKA HILI ..’AUVAMIA’ UONGOZI…


UONGOZI wa klabu ya Azam Fc umewatimua kazi benchi zima la klabu hiyo baada ya kutoka sare 0-0 dhidi ya Kagera Sugar mchezo uliochezwa jana katika uwanja wa Chamazi.

Benchi la Azam linaongozwa na kocha mkuu George Lwandamina na msaidizi wake Bahati Vivier.

Gazeti la Mwanaspoti baada ya kuzipata taarifa hizo lilimtafuta Lwandamina na alikiri kupokea taarifa hizo huku akiweka wazi yupo njiani kwenda kuonana na mabosi wake.

“Nimepokea taarifa hiyo lakini naenda kuonana na viongozi wa klabu, ni maisha yetu ya mpira,” amesema Lwandamina.

Kocha huyo mwezi uliopita alitoka kuongezewa mwaka mmoja wa kuendelea kuiongoza timu hiyo lakini mabosi wake wameamua kuuvunja mkataba huo.

Azam mpaka sasa wanashika nafasi ya saba wakiwa na pointi 11 waishinda mechi tatu,  sare mbili na kupoteza mechi tatu.

SOMA NA HII  HII NDIO FURAHI DAY SASA SINGIDA FG vs YANGA