Home news KISA KUTAKIWA KURUDI YANGA…METACHA MNATA ATEMANA NA WAKALA WAKE…

KISA KUTAKIWA KURUDI YANGA…METACHA MNATA ATEMANA NA WAKALA WAKE…


Golikipa namba moja wa Timu ya Polisi Tanzania, Metacha Mnata amevunja mkataba na aliekuwa meneja wake Jemedari Said.

Tamko hili limekuja wakati huu ambapo metacha anazungumzwa kuhitajika na Yanga ambao wanampoteza Golikipa wao raia wa Mali Diarra anaekwenda kujiunga na Timu yake ya Taifa katika michuano ya AFCON.

Uhusiano wa Meneja huyo na Viongozi wa Yanga kwa siku za hivi karibuni umekuwa sio wa kuridhisha jambo linalowaacha wengi na maswali pengine ili aweze kurudi Yanga kwa urahisi basi golikipa huyo ameona ni vyema aachane na meneja wake.

SOMA NA HII  WALIOPIGWA GOLI 9-0 NA AZAM FC...WAIBUKANA HAYA MAPYA...WAMTAJA MANDONGA....