Home Azam FC KUELEKEA MECHI DHIDI YA SIMBA…AZAM FC WAFANYA MAAMUZI MAGUMU…

KUELEKEA MECHI DHIDI YA SIMBA…AZAM FC WAFANYA MAAMUZI MAGUMU…

 


OFISA Habari wa Azam FC, Thabiti Zakaria amefunguka na kuelezea maandalizi yao ya kuwamaliza Simba kwenye mchezo wao wa Ligi Kuu Bara.

Mchezo huo unatarajiwa kupigwa Januari Mosi, mwakani huku Simba wakiwa wenyeji wa Azam katika Uwanja wa Mkapa, Dar.

Kwenye michezo yao ya mwisho ya Ligi Azam alimpiga Ruvu Shooting mabao 4-1, huku Simba akimpiga KMC 4-1.

Kwenye msimamo Ligi Kuu Bara, Azam ipo nafasi ya saba kwa alama 15, Simba ikiwa nafasi ya pili kwa alama 21. Kinara akiwa Yanga mwenye alama 23 kabla ya mechi za jana.

Akizungumza na Gazeti la Championi , Zakaria amesema: “Tunaanza mazoezi kesho (leo) maana wachezaji walipata mapumziko baada ya mchezo wetu na Ruvu Shooting.

“Mazoezi yetu tutakuwa tunafanya usiku saa moja maana ndiyo muda wa mechi yetu na Simba.

“Siku zote si rahisi haswa timu kubwa zinapokutana ila sisi kwa upande wetu tumejiandaa na ushindi.

“Wachezaji watakaokosekana kwenye mchezo huo ni Iddy Nado ambaye matatizo yake yanajulikana kuwa yupo nje kwa miezi tisa na Ayoub Lyanga.”

SOMA NA HII  DAKIKA CHACHE KABLA YA KUKIPIGA NA SIMBA LEO...KIIZA AIBUKA NA HILI KUHUSU KAGERA SUGAR....