Home news KUELEKEA MECHI DHIDI YA SIMBA..SENZO AIBUKA NA JAMBO YANGA..AWANYOOSHEA KIDOLE WACHEZAJI…

KUELEKEA MECHI DHIDI YA SIMBA..SENZO AIBUKA NA JAMBO YANGA..AWANYOOSHEA KIDOLE WACHEZAJI…


Wachezaji wa Young Africans wamepewa mapumziko ya siku mbili, kabla ya kurejea kambini kuanza maandalizi ya mchezo wa Mzunguuko wanane wa Ligi Kuu Tanzania Bara utakaowakutanisha na watani zao wa jadi Simba SC.

Young Africans itacheza dhidi ya Simba SC Desemba 11, katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, huku wakichagizwa na ushindi wa 1-0 walioupata kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii mwezi Septamba.

Baada ya kikosi cha vinara hao wa Ligi kuu kuwasili jijini Dar es salaam, kikitokea jijini Mbeya, Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Young Africans Senzo Mazingisa amesema katika kikao cha benchi la ufundi na wao kama uongozi wamekubaliana kuwapa mapumnziko ya siku mbili wachezaji wao baada ya ushindi huo.

Senzo amesema baada ya mapumziko hayo kikosi chao haraka kitarejea kambini kuanza maandalizi ya mchezo unaofuata dhidi ya Simba utakaopigwa Desemba 11 katika Uwanja wa Mkapa.

“Tumeona wachezaji nao wakazione familia zao katika hizi siku mbili na baada ya mapumziko hayo tutarejea kazini kuanza kujipanga na mchezo huo unaokuja dhidi ya watani wetu Simba,”amesema Senzo.

Aidha Senzo amesema kuanzia uongozi wao,wachezaji na makocha wanatamani matokeo ya ushindi katika mechi hiyo kubwa inayokuja na kwamba maandalizi yao yatakuwa yenye uzito unaostahili.

“Achana na sisi viongozi wachezaji wetu wanajua umuhimu wa ushindi katika mechi hii na hata makocha wao kwahiyo tutakuwa na maandalizi yanayolingana na uzito wa hii mechi tunakiamini kikosi chetu.”

Young Africans jana Jumanne (Novemba 30), ilicheza dhidi ya Mbeya Kwanza FC mjini Mbeya katika Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine na kuibuka na ushindi wa mabao 2-0.

Ushindi huo unaendelea kuiweka kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara klabu hiyo kongwe katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati kwa kufikisha alama 19, ikifuatiwa na Simba SC yenye alama 14.

SOMA NA HII  KISA DIARRA..YANGA YAMVUTIA KASI MAKAKA WA RUVU SHOOTING...MPANGO MZIMA UKO HIVI..