Home news KUHUSU ‘SURE BOY’ KUMALIZANA NA YANGA..BABA’KE ASHINDWA KUJIZUA..AFUNGUKA HAYA…ATAJA MGOGORO..

KUHUSU ‘SURE BOY’ KUMALIZANA NA YANGA..BABA’KE ASHINDWA KUJIZUA..AFUNGUKA HAYA…ATAJA MGOGORO..


BABA mzazi wa kiungo wa Azam FC, Salum Aboubakar ‘Sure Boy’, mzee Aboubakar Salum ‘Sure Boy Sr’ ameweka wazi kuwa mtoto wake yupo mbioni kumalizana na mabosi wa Yanga baada ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuvunja mkataba wa mchezaji huyo na Azam FC kutokana na mgogoro uliokuwepo.

Kiungo huyo ni miongoni mwa wachezaji watatu wa Azam FC waliosimamishwa kwa utovu wa nidhamu. Wengine ni Agrey Morris na Mudathir Yahya.

Akizungumza na Spoti Xtra, mzee Aboubakar alisema mtoto wake amebakisha asilimia chache za kujiunga na Yanga baada ya kufikia makubaliano kwenye mambo mengi ya msingi huku akienda mbali akisema tayari mkataba wake na Azam umeshavunjwa na TFF.

“Nilianza kusikia kwenye vyombo vya habari lakini tayari kijana mwenyewe amenieleza kila kitu juu ya Yanga, tayari wameshakubaliana vitu vingi na mabosi wa Yanga kwa ajili ya kusaini mkataba baada ya TFF kuuvunja mkataba wake na Azam kutokana na mgogoro wao wa muda mrefu.

“Nadhani kwa sasa watakuwa wamebakisha mambo machache ya kimasilahi kabla ya kumalizana kabisa, suala ya yeye kwenda kwenye timu ambayo nilicheza kwangu ni jambo zuri japokuwa sikutaka iwe hivyo, ila kutokana na matatizo yake na Azam imekuwa ni jambo kubwa.

“Yanga kuna wachezaji wengi wazuri, suala la yeye kucheza itategemea na mwalimu atatumia mfumo gani, ila naamini atacheza tu,” alisema Sure Boy Sr.

SOMA NA HII  EDO KUMWEMBE: VIONGOZI SIMBA SC WANAPAMBANA KUIVUNJA TIMU YAO...WANATAKA IONEKANE KAMA PRISONS TU....