News

KISA USAJILI WA NKANE…NABI APANGA KUPITISHA PANGA YANGA…KASEKE AWEKWA KWENYE ‘RED ZONE’…

admin January 4, 2022 6:00 am


Kiungo Mkongwe Deusi Kaseka huenda akaguswa na maamuzi ya Benchi la Ufundi la Young Africans ya kumtoa kwa mkopo mmoja wa viungo wa klabu hiyo.

Usajili wa kiungo Denis Nkane unalazimisha kufanywa kwa maamuzi ya kiungo mmoja kuondoka klabuni hapo kwa mkopo katika kipindi hiki cha Dirisha Dogo La Usajili.

Imefahamika kuwa Kaseke ambaye hapati nafasi ya kucheza mara kwa mara ataguswa na uamuzi huo ambao umeshapewa baraka na Kocha Mkuu Nasreddine Nabi.

Kocha huyo kutoka Tunisia amesema usajili wa kiungo Dennis Nkane aliyetokea Biashara United Mara unamsukuma kufanya maamuzi hayo ya kumpunguza mchezaji mmoja.

“Kwa sasa tutakuwa na jumla ya mawinga watano, naangalia uwezekano wa kumtoa mmoja ili timu iwe na uwiano mzuri tubaki na wanne.”

Mbali na Nkane, mawinga wengine ni Farid Mussa, Dickson Ambundo, Jesus Moloko na Deus Kaseke.

NABI AMCHOMOA MUKOKO SIMBA..NKANE ATISHIWA NA SIMU YANGA..SIMBA HII UNAPIGWA NYINGI… SIMBA WAZIDI KUKIMBIZA ‘MWIZI KIMYA KIMYA’..YASHUSHA KIFAA CHA WYADAD CASABLANCA YA MOROCCO….

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply