News

MKWASA ‘ALA MATAPISHI YAKE’ RUVU SHOOTING…MASAU BWIRE AVUNJA UKIMYA..AANIKA YOTE…

admin January 4, 2022 3:00 pm


Klabu ya Ruvu Shooting imethibitisha kurejea kwa Kocha Mkuu Charles Boniface Mkwasa aliyekua ametangaza kujiuzulu nafasi hiyo tangu juma lililopita.

Mkwasa alitangaza kujizulu nafasi yake klabuni hapo siku moja baada ya kikosi cha Ruvu Shooting kupoteza mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Azam FC kwa kufungwa mabao 4-1.

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasilino ya Klabu hiyo yenye Maskani yake Makuu mjini Mlandizi mkoani Pwani Masau Bwire amesema, Kocha Mkwasa amerejea kwenye majukumu yake na tayari amefanya usajili wa wachezaji sita katika kipindi hiki cha Dirisha Dogo la Usajili.

“Charles Boniface Mkwasa amerejea kwenye majukumu yake ndani ya kikosi cha Ruvu Shooting, na tayari tumeshakamilisha sajili za wachezaji sita ambao tayari wapo kambini.” amesema Masau Bwire.

Baada ya kutangaza kujiuzulu nafasi ya Kocha Mkuu, Mkwasa alitoa sababu za kufanya hivyo kwa kusema kilichomsukuma kuondoka Ruvu Shooting ni matokeo mabovu, tangu walipoanza msimu huu 2021/22.

IMEVUJA…HII NI ZAIDI YA KUFURU…HUO MKATABA WA MSHERY NA YANGA NI WA KIULAYA ULAYA ZAIDI… SHIBOUB AANZA KUKIWASHA NA SIMBA ZANZIBAR…PABLO AMWEKA KWENYE ‘LISTI’…HUYO MUAIVORY MHH…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply