Shirikisho lenye dhamana ya kuongoza soka ulimwenguni (FIFA) imeiamuru klabu ya CS Constantine kumlipa fedha anazodai Kiungo walieachana nae, Sharaf Eldin Shaiboub Ali Abdelrahman ndani ya siku 45 hii ni baada ya kumvunjia mkataba wake.
Klabu hiyo inayoshiriki ligi kuu ya Algeria, inapaswa kumlipa Shaiboub dola za kimarekani 140,000 sawa sawa na Tshs.322,980,000, kinyume na hapo itafungiwa kusajili kwa madirisha kadhaa ambayo bado hayajawekwa wazi.
Shaiboub, alijiunga na Constantine msimu wa 2020/2021 akitokea Simba alipohudumu kwa mwaka mmoja akishinda mataji matatu ya FA, Ngao ya Jamii na Ligi kuu Tanzania Bara.
Kwa sasa raia huyo wa Sudan, yupo visiwani Zanzibar akiwa na Simba kwaajili ya majaribio na iwapo atafanya vizuri atafanikiwa kusajiliwa na mabingwa hao wa soka nchini.
Vile vile Shaiboub amecheza michezo nane kwenye timu yake ya Taifa ya Sudan, akiwa bado hajafanikiwa kufanga bao lolote.