Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Senegal Pappe Ousmane Sakho amekubali kubadilisha namba ya jezi aliyokua akiitumikia tangu mwanzoni mwa msimu huu alipotua klabuni hapo, na kumuachia Kiungo Mwenzake kutoka nchini Zambia Clatous Chotta Chama ambaye tayari ameshatangazwa kurejea kwenye klabu hiyo akitokea RS Berkane ya Morocco.
Mmoja wa viongozi wa Simba SC ambaye hakutaka jina lake litajwe hadharani amesema, baada ya Sakho kukubali kumuachia Chama namba 17, yeye atavaa namba 10 ambayo ilikua inatumiwa na Kiungo Ibrahim Ajib aliyetimkia Azam FC kufuatia mkataba wake kuvunjwa klabuni hapo.
“Ombi la Chama limekubaliwa baada ya Pape Ousmane Sakho kukubali kumwachia Chama jezi namba 17 huku yeye akiomba kuvaa namba 10 iliyokuwa ikivaliwa na Ibrahim Ajibu,” amesema kiongozi huyo