News

CHAMA AITEKA SOKOINE…UWANJA MZIMA WALIPUKA JINA LAKE..PABLO AWAKATA MAINI…

admin January 17, 2022 12:38 pm

 


”Chama, Chama, Chama, Chama”. Ni shangwe na kelele zilizosikika kwa mashabiki wakimlaki nyota wao raia wa Zambia, Clatous Chama wakati Simba ikiwasili uwanja wa Sokoine tayari kwa mchezo wao dhidi ya Mbeya City.

Shangwe hizo zilitokea wakati timu hiyo ikitua kwa ajili ya maandalizi ya mwisho kuwakabili wenyeji Mbeya City katika mchezo wa Ligi Kuu utakaopigwa saa 10:00 jioni.

Mbeya City ndio walitangulia kutua saa 7:44 mchana bila amsha amsha yoyote wakipigiwa makofi na mashabiki wao hadi vyumba vya kubadilishia nguo.

Saa 8:17 Simba ilitinga uwanjani hapo ikiongozwa na gari la Polisi na kuamsha mzuka uliojaa shangwe kwa mashabiki walianza kuliimba jina la Mwamba huyo wa Lusaka.

Hata hivyo katika sura zilizoshuka kwenye gari la wachezaji, staa huyo hakuwa miongoni lakini viongoni walinong’onezana na kumshusha nje ili kuwapungia mkono mashabiki.

Hatua hiyo iliamsha yowe kwa wakereketwa hao waliojaa jukwaani wakishangilia, huku Afisa Habari wa timu hiyo, Ahmed Ally naye akiongeza mzuka kwa mashabiki.

KWA SIMBA HII….LITAKUFA JITU JAMENI…CHAMA AFUNGUKA KILA KITU.. SIMBA WAANGUKIA PUA MBEYA…YAPIGWA KIMOJA CHA UCHUNGU CHWAAA…PABLO ALAMBWA KADI YA NJANO…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply