news

KIWANGO CHA CHAMA CHAZUA GUMZO MORO…PABLO APAGAWA..AMPA RASMI MAJUKUMU MAPYA…

admin January 21, 2022 6:05 pm


KIUNGO wa Simba, Clatous Chama ameanza kuwapa raha mashabiki wake mapema baada ya kupiga pasi zinazofika eneo husika.

Kocha wa Simba, Pablo Franco aliwapanga Chama, Rally Bwalya na Bernard Morrison kupiga mashuti nje ya 18, pia kupika kona.

Chama alifikisha mashuti yake eneo linalotakiwa, jambo ambalo liliwapa raha mastaa wenzake.

Pablo ni kama anamkabidhi majukumu Chama ya kupiga faulo, kwani amewatenga pembezoni mwa uwanja kupiga faulo, akiwa na Bwalya.

Kwa namna kocha anavyompa majukumu Chama ni dhahiri atampanga mchezo wa kesho Jumamosi dhidi ya Mtibwa Sugar, ambao utapigwa Manungu.

Chama alipiga shuti kwa Hassan Dilunga ambaye alitokea katikakati la kundi la wachezaji wengine, huku Meddie Kagere,Chris Mugalu na Sakho wakikimbia kufunga.

Amewatenga mabeki Joash Onyango,Juma Kennedy na Inonga kuwawahi kina Kagere mbele.

BAADA YA KUICHEZEA YANGA KWA MARA YA KWANZA..CHICO AIKISA KICHWA..KISHA AKANENA HAYA MAZITO… KISA KIPIGO KUTOKA MBEYA CITY…PABLO AVUNJA UKIMYA SIMBA..AFUNGUKA ALIYOTARAJIA…AWATAJA WACHEZAJI..

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply