Home news BAADA YA KUIUA SIMBA…STRAIKA WA MBEYA CITY APIGIWA SIMU NA YANGA..AANIKA ALICHOAMBIWA..

BAADA YA KUIUA SIMBA…STRAIKA WA MBEYA CITY APIGIWA SIMU NA YANGA..AANIKA ALICHOAMBIWA..


MSHAMBULIAJI wa Mbeya City, Paul Nonga, amefichua kuwa kitendo cha kufanikiwa kuwafunga Simba katika mchezo wa Ligi Kuu Bara, kimesababisha apokee simu nyingi za pongezi, zikiwemo za baadhi ya watu wa Yanga.

Nonga, ambaye pia aliwahi kuchezea Yanga, bao lake la Jumatatu iliyopita katika mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Simba, lilitosha kumchinja Mnyama na kuipa Mbeya City ushindi wa bao 1-0. Hiyo ilikuwa ni mara ya kwanza Simba wanafungwa kwenye ligi msimu huu.

Akizungumza na Gazeti la Championi Ijumaa, Nonga alisema baada ya mchezo huo, alipokea simu nyingi za pongezi kutoka kwa wadau mbalimbali wa timu hiyo wakiwemo watu wa Yanga ambao wamekuwa ni mahasimu wakubwa wa Simba katika Ligi Kuu Bara.

“Kitu kikubwa ambacho kilitokea baada ya matokeo ya ushindi dhidi ya Simba, ni kwamba nilipokea simu nyingi za pongezi kutoka kwa wadau mbalimbali wa Mbeya City, kwa sababu tulijiandaa kupata matokeo ingawa sikupokea simu za wadau wa Mbeya City peke yake, kwani hata watu wa Yanga wapo wengi ambao walinipigia simu za pongezi kutokana na ushindi ambao tuliupata.

“Unajua Yanga na Simba ni mahasimu halafu inakuwa ni kawaida ikitokea Simba au Yanga ikifungwa na hizi timu nyingine, mashabiki kuchekana na kwangu ilikuwa hivyo kwa kuwa kwao wao ni jambo la kawaida halafu ndiyo maisha ya soka jinsi yanavyokwenda wakati wote ila jambo kubwa kwa sasa tunaangalia mechi nyingine ambazo zipo mbele yetu,” alisema Nonga.

SOMA NA HII  KWA TAARIFA YAKO...MAYELE NA KAGERE NI KITU KIMOJA...WOTE WAZEE WA KUTETEMA , WABAYA WA DK ZA JIONI...