Home news AMBUNDO AWAMBUNDUA POLISI TZ..YANGA WAVUNJA MWIKO ..HUYO CHICO MMHHHH…

AMBUNDO AWAMBUNDUA POLISI TZ..YANGA WAVUNJA MWIKO ..HUYO CHICO MMHHHH…


Mshambuliaji wa Yanga Fiston Mayele na winga Dickson Ambundo,   wamejikuta wakitengeneza pacha safi la maangamizi hadi kuzaa bao la ushindi kwa Yanga dakika ya 64.

Pacha hiyo imeonekana katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC, Kati ya Polisi Tanzania waliowakaribisha Yanga katika Uwanja wa Sheikh Amri abeid, Arusha.

Timu hizo zilizoenda hadi mapumziko bila kucheka na nyavu, kipindi cha Pili hali ikawa shwari kwa wageni Yanga baada ya Mayele kuanzisha mashambulizi ya mbali  kuelekea golini kwao na Ambundo na kufuatilia moto huo huo, hadi ndani ya 18 alipopokelea pasi safi na kuweka mpira nyavuni.

Shambulizi hilo lililozaa bao la kuongoza kwa Yanga  dakika ya 64, limeinua mashabiki waliokuwa wakiimba kwa unyonge wa hofu ya sare, na kuongeza shangwe zaidi majukwaani.

Katika mchezo huo, kiungo mpya Chico Ushindi alipata nafasi pia ya kucheza, ambapo tofauti na matarajio ya wengi, alionekana kuwa mzito na mwenye kukos utulivu hali iliyochangiwa na ugeni wa Ligi.

Yanga imeongeza gepu kubwa kati yake na anayemfuatia baada ya kufikisha pointi 35 huku anayemfuatia Simba yenye pointi 25.

SOMA NA HII  LICHA YA GOLI LA KANOUTE 'KUUA MTU' JANA....HIZI HAPA DONDOO MUHIMU ZA AJABU KATI YA SIMBA vs COASTAL..