Home news EHEE…KUMBE HII NDIO SABABU YA BARBARA KUSOTA POLISI KWA ZAIDI YA LISAA...

EHEE…KUMBE HII NDIO SABABU YA BARBARA KUSOTA POLISI KWA ZAIDI YA LISAA …MWENYEWE APIGA KIMYA YANI…


MTENDAJI Mkuu (C.E.O) wa Simba, Barbara Gonzalez juzi Ijumaa alilazimika kusota kwa saa zima kwenye Kituo Kikuu cha Polisi (Central) Dar, baada ya kuitwa kwa ajili ya kesi yake inayomkabili dhidi ya Ofisa wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jackline Kamwamu.

Gazeti la Championi ambalo lilikuwepo kituoni hapo lilimshuhudia Barbara akifika kituoni hapo saa 9:10 alasiri akiwa kwenye gari lake kabla ya kushuka nje ya kituo hicho na kuingia ndani kisha kutoka saa 10:15 jioni, akitumia saa moja kituoni hapo.

Barbara alifunguliwa kesi ya udhalilishaji na ofisa huyo wa TFF kwa madai ya kumdhalilisha wakati akijaribu kumzuia asiingie kwenye eneo VVIP katika mechi ya Ligi Kuu Bara kati ya Simba na Yanga Desemba 11, mwaka jana.

Hii ni mara ya pili kwa Barbara kuitwa polisi kutokana na kesi hiyo baada ya mara ya kwanza wiki iliyopita kushikiliwa katika kituo cha polisi Alhamisi iliyopita na kumfanya ashindwe kuwepo kwenye mechi ya Simba dhidi ya Mtibwa Sugar.

CEO huyo baada ya kutoka kituoni humo hakutaka kuzungumza na vyombo vya habari bali alipanda kwenye gari lake na kuondoka.

SOMA NA HII  KISA UCHAGUZI ...KADUGUDA ALIAMSHA SIMBA SC...AANIKA SAFARI YA BARBARA QATAR..