Home news EHEE…KUMBE ISHU YA MUKOKO KUTUA MAZEMBE ILIKUWA HIVI BANA…MAKUBWA YAFICHUKA..ALIGOMA…

EHEE…KUMBE ISHU YA MUKOKO KUTUA MAZEMBE ILIKUWA HIVI BANA…MAKUBWA YAFICHUKA..ALIGOMA…


Nahodha msaidizi wa Yanga, Mukoko Tonombe ameondoka rasmi ndani ya viunga hivyo baada ya kusaini miaka miwili TP Mazembe.

Kiungo huyo ametua kwa matajiri hao wa Congo baada ya kuhusishwa nao kwa muda mrefu na hatimaye yametimia.

Hapo awali ilisemekana dili la kiungo huyo kwenda Mazembe lilikufa baada ya kugoma kutolewa kwa mkopo katika klabu hiyo na kutaka kuuzwa.

Mabosi wa Yanga tayari walikuwa washakubaliana na mchezaji huyo kwenda Mazembe baada ya kuona hapati nafasi katika kikosi cha kwanza cha Nasreddine Nabi na pia kupata nafasi ya kumleta winga, Chico Ushindi ambaye alitua klabuni hapo akitokea TP Mazembe.

Katika dili la Yanga kumtaka Chico walitaka kumpeleka Mukoko kwa mkopo ili kumpata winga huyo. 

SOMA NA HII  BAADA YA KUTAMBULISHWA...RONALDO AANZA KUWAPA MASHARTI WAARABU...