Home news FT: AZAM FC 0-1 SIMBA ….SIMBA WABEBA KOMBE KIBABE…MKUDE AMPAGAWISHA RAIS MWINYI...

FT: AZAM FC 0-1 SIMBA ….SIMBA WABEBA KOMBE KIBABE…MKUDE AMPAGAWISHA RAIS MWINYI KWA STORI…


SIMBA ni mabingwa wa Kombe la Mapinduzi 2022 wanachukua kombe Uwanja wa Amaan ikiwa ni taji lao la nne.

Dakika 90 zinakamilika kwa ubao kusoma Azam FC 0-1 Simba na mtupiaji ni Meddie Kagere aliyefunga bao hilo kwa mkwaju wa penalti.

Tepsi Evans wa Azam FC amepewa zawadi ya kuwa mchezaji bora muungwana huku Henock Inonga wa Simba akitwaa tuzo ya mchezaji bora wa mchezo.

Hili linakuwa taji la nne kwa Simba huku Azam FC ikiwa imetwaa mataji matano na ni mabingwa wa kihistoria wa Kombe la Mapinduzi.

Aidha katika moja ya tukio la mechi hiyo lililovuta hisia ni pale Kiungo wa Simba, Jonas Mkude alipoonekana akipiga stori na kumfurahisha Mgeni Rasmi, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe Hussein Ally Hassan Mwinyi.

SOMA NA HII  KUHUSU KIWANGO CHA SIMBA MSIMU HUU...VICTOR COSTA AIBUKA NA HILI...ADAI KUNA KITU KIMEJIFICHA...