Home Uncategorized AZAM FC BANA, WAIVUTIA KASI FRIENDS RANGERS

AZAM FC BANA, WAIVUTIA KASI FRIENDS RANGERS

MABINGWA watetezi wa Kombe la Shirikisho, Azam FC, Jana wameanza mazoezi ya kuivutia kasi timu ya Friends Rangers kuelekea kwenye mchezo wao wa hatua ya 32 bora utakaochezwa Januari,27, Uwanja wa Uhuru.
Azam FC, iliiyo chini ya Kocha Mkuu, Arstica Cioaba ilitwaa kombe hilo kwa kuifunga Lipuli FC, bao 1-0 lililofungwa na Obrey Chirwa kwenye mchezo wa fainali.
Akizungumza na Saleh Jembe, Kocha Msaidizi wa Azam FC, Idd Cheche alisema kuwa kikubwa wanachokifanya kwa sasa ni kuandaa kikosi kazi kitakachoendeleza safari ya kutetea taji lao la Shirikisho.
“Ukiwa bingwa mtetezi inamaanisha kwamba kila mechi kwako ni fainali, kikubwa ambacho tunakitazama kwa sasa ni kuona namna gani tunapata ushindi mbele ya Friends Rangers, ni timu bora tunaiheshimu hivyo tutapambana kutafuta matokeo chanya,” amesema Cheche.
SOMA NA HII  MTAMBO WA KAZI YANGA, SAIDO NTIBANZOKIZA KUANZA KUONYESHA MAKEKE LEO