Home Habari za michezo GAMONDI AFUNGUKA MIPANGO YAKE KWENYE KUIFUA YANGA

GAMONDI AFUNGUKA MIPANGO YAKE KWENYE KUIFUA YANGA

KATIKA kuhakikisha wanafanikiwa na kushinda kila mechi, Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi amesema kutokana na mfumo anaoutumia kila mchezaji anaweza kufunga mabao sio lazima mshambuliaji peke.

Yanga hadi sasa ameshacheza mechi tisa  wakitikisa nyavu mara 26, Stephen Aziz Ki na Max Nzengeli wakiwa vinara wa kufunga ndani ya timu hiyo kila mmoja akitikiza nyavu mara 7  na manne yakifungwa na Pacome Zouzoua

Washambuliaji Hafiz Konkoni na Clement Mzize kila mmoja amefunga mabao mawili  na Mudathiri Yahya na Dickson Job kila mmoja akifunga moja.

Kocha huyo amesema mipango yake katika kufundisha anawapa uhuru wachezaji wake wake hasa mwenye uwezo wa kutumia nafasi anaweza kufunga na sio lazima mshambuliaji.

Amesema wachezaji wote wana kazi ya kupambania uwanjani ili kutafuta ushindi, na lazima kila mtu kuwa makini kutumia vizuri nafasi zinazopatikana bila kujali anacheza nafasi gani.

“Mipango yangu kila mchezaji anatakiwa kutumia nafasi zinazopatikana akiwa sehemu nzuri  kufunga anaweza anatakiwa kufanya jukumu hilo, kila mtu yupo huru kupambania timu inapata matokeo chanya.

Ukiangalia mabao tuliyofunga mengi yamefungwa na viungo, washambuliaji hawajafunga mabao mengi, hii ni jinsi gana ninavyotaka kwa wachezaji wangu hasa katika kushirikiana katika kutimiza majukumu,” amesema kocha huyo.

Ameongeza kuwa viungo wanafunga mabao mengi na mabeki watafanya hivyo kwa kuwa anawapa uhuru wa kufunga ili kuipa timu matokeo mazuri ili kufikia malengo yao.

Gamondi alimesistiza kuwa anahitaji kuoata matokeo mazuri katika kila mechi jambo ambalo wachezaji wake wanatambua na kila mmoja kuhakikisha anatumiza majukumu anayopewa siku ya mechi.

Kuhusu maandalizi ya mchezo ujao wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya CR Belouizdad, Algeria, alisema mazoezi yanaendelea kwa wachezaji ambao hawako kwenye majukumu ya timu za taifa.

“Tumefanikiwa kuwaangalia wapinzani wetu baadhi ya mechi zao na kuona ubora wao kikibwa ni maandalizi yetu kuelekea mchezo huo ni muhimu kupata matokeo mazuri ugenini,” amesema Gamondi.

SOMA NA HII  KAKOLANYA ATOA TAMKO JUU YA NAFASI YAKE SIMBA