Home Habari za michezo WAKATI MAMBO MENGINE YAKIENDELEA HUKO SIMBA, KIKOSI KIMESHUKA KAMBINI LEO KWAAJILI HII

WAKATI MAMBO MENGINE YAKIENDELEA HUKO SIMBA, KIKOSI KIMESHUKA KAMBINI LEO KWAAJILI HII

WAKATI uongozi wa Simba ukiendelea na mchakato wa kuziba nafasi ya benchi la ufundi, Kaimu Kocha Mkuu wa Simba Daniel Cadena amesema wameanza maandalizi ya kukisuka kikosi chao kuelekea mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Asec Mimosas ya Ivory Coast.

Simba imeingia kambini leo asubuhi kwa wachezaji ambao hawako kwenye majukumu ya timu za taifa kuendelea na maandalizi ya mchezo wa kwanza wa hatia ya makundi ya Ligi ya Mabingwa utakaochezwa Novemba 25, mwaka huu uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam.

Cadena anashirikiana na Seleman Matola kuimarisha kikosi cha timu hiyo huku wakiendelea kuwafatilia wapinzani wao Asec Mimosas ili kupata matokeo mazuri katika mchezo wa kwanza.

Kocha Daniel amesema baada ya kutopata matokeo mazuri katika michezo miwili iliyopita ya Ligi Kuu Bara  wameona madhaifu yao na kuanzia kufanyia kazi.

“Kazi kubwa kuendelea kujiimarisha safu ya ulinzi kutoruhusu mabao na ushambuliaji kuwa makini na utulivu kwenye nafasi wanazotengeneza na kupata mabao.

Mechi iliyopita na Namungo FC tulitengeneza nafasi  hatujazitumia na sasa tunaanzia hapo kufanyia kazi kwa washambuliaji wetu na kuwasisiza mabeki kuwa na utulivu ili kutorudia makosa hayo,” amesema Daniel.

Naye Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally amesema mchakato wa kutafuta Kocha Mkuu unaendelea, wiki hii watamtambulisha  rasmi mrithi wa Robertinho.

Ameongeza kuwa wanametafuta kocha aliyekuwa bora na uzoefu mkubwa na soka la Afrika ili kuweza kusaidia Simba kufikia malengo yao katika mashindano ya ndani na kimataifa.

Ahmed amesema kikosi kimeingia kambini jana kwa wachezaji ambao hawako kwenye majukumu ya timu ya Taifa kuendelea na maandalizi ya mchezo ujao dhidi ya Asec Mimosas.

SOMA NA HII  MAXI, AZIZ KI WAIPONZA SIMBA, MILIONI 300 ZIMEPITA HIVI