Home Habari za michezo SIMBA IMEBADILIKA KILA KITU…. TATIZO BADO LIKO HAPA

SIMBA IMEBADILIKA KILA KITU…. TATIZO BADO LIKO HAPA

Habari za Simba

Mchambuzi wa soka Bongo George Ambangile amesema Simba SC imebadilika kutoka ile iliyokuwa inaruhusu sana magoli na kilichobaki ni kupachika magoli kwenye nyavu.

Ambangile ametoa maoni hayo alipokuwa akiichambua mechi ya Simba dhidi ya Jwaneng Galaxy ambayo iliisha kwa sare ya 0-0.

“Simba walikabia juu, Saido, Kibu na Baleka walianza kukaba vizuri kuanzia juu lakini sio hao tu viungo wakabaji Kanoute na Ngoma walisogea, vilevile mabeki wa pembeni walisogea juu na kuwafanya Jwaneng waanze kupiga mipira mirefu.

“Nimeona Simba imebadilika na hii ni meseji nadhani kutoka kwa Kocha Benchikha kwamba usipojitoa kukaba unapoteza namba,” alisema Ambangile.

SOMA NA HII  SIMBA HAKUNA KUCHEKA KWA SASA, MWENDO WA DOZI KUTWA MARA TATU