Home Habari za michezo MTEGO WA CHAMA DHIDI YA WYDAD UMEKAA HIVI

MTEGO WA CHAMA DHIDI YA WYDAD UMEKAA HIVI

Habari za SImba SC

Kiungo mshambuliaji Clatous Chama anajadiliwa kwamba huwenda akaanza kwenye mchezo dhidi ya Wydad kutokana na kila alichokionesha kwenye mchezo dhidi ya Jwaneng Galaxy.

Mchambuzi wa soka George Ambangile amelizungumzia hilo na kusema, mwalimu wa Simba Benchikha atakuwa ameshategeua kitendawili hicho sababu tayari ameshaanza kuwafahamu vizuri wachezaji wake.

“Angalau sasa hivi anaweza kuwa amewajua wachezaji wake, anaweza kuangalia nini afanye kulingana na mbinu zake. Chama na Saido wote ukiwaambia wacheze pembeni au namba kumi, watakuwambia wanataka namba kumi sasa utaona hapo ni jinsi gani kocha atatakiwa kuwa na maamuzi magumu.

“Anaweza kuaanzisha wote lakini akatoa maelekezo kwa mmoja wao kuwa na jukumu la kukaba zaidi au vinginevyo,” alisema Ambangile.

Kwenye mechi iliyopita ya Jwaneng, winga moja alicheza Kibu Denis na nyingine akacheza Onana lakini hata hivyo, waliweza kuzuia vizuri na kushambulia lakini hawakuweza kupata matokeo.

Alipoingia Chama, alionesha kuwa na maarifa zaidi ya kupata matokeo kwa kupiga shuti zuri lililoenda kugonga mwamba lakini hata hivyo kuonesha ana madhara zaidi karibu na goli hivyo tutaona mechi dhidi ya Wydad Benchikha ataamua nini.

SOMA NA HII  KOCHA MPYA BARCA AWAFUNGULIA MLANGO SUAREZ, BUSQUETS, JORDI ALBA