Home news KISA USAJILI WA NKANE…NABI APANGA KUPITISHA PANGA YANGA…KASEKE AWEKWA KWENYE ‘RED ZONE’…

KISA USAJILI WA NKANE…NABI APANGA KUPITISHA PANGA YANGA…KASEKE AWEKWA KWENYE ‘RED ZONE’…


Kiungo Mkongwe Deusi Kaseka huenda akaguswa na maamuzi ya Benchi la Ufundi la Young Africans ya kumtoa kwa mkopo mmoja wa viungo wa klabu hiyo.

Usajili wa kiungo Denis Nkane unalazimisha kufanywa kwa maamuzi ya kiungo mmoja kuondoka klabuni hapo kwa mkopo katika kipindi hiki cha Dirisha Dogo La Usajili.

Imefahamika kuwa Kaseke ambaye hapati nafasi ya kucheza mara kwa mara ataguswa na uamuzi huo ambao umeshapewa baraka na Kocha Mkuu Nasreddine Nabi.

Kocha huyo kutoka Tunisia amesema usajili wa kiungo Dennis Nkane aliyetokea Biashara United Mara unamsukuma kufanya maamuzi hayo ya kumpunguza mchezaji mmoja.

“Kwa sasa tutakuwa na jumla ya mawinga watano, naangalia uwezekano wa kumtoa mmoja ili timu iwe na uwiano mzuri tubaki na wanne.”

Mbali na Nkane, mawinga wengine ni Farid Mussa, Dickson Ambundo, Jesus Moloko na Deus Kaseke.

SOMA NA HII  KAMBI YA SIMBA MOROCCO IMEZUA JAMBO HILI