Home news STAA WA YANGA ACHEKELEA MATOKEO YA SIMBA MBEYA…AWAPONGEZA..AWAOMBEA MATOKEO ZAIDI…

STAA WA YANGA ACHEKELEA MATOKEO YA SIMBA MBEYA…AWAPONGEZA..AWAOMBEA MATOKEO ZAIDI…


SIMBA imepooza machungu ya jeraha la beki wa Yanga, Abdallah Shaibu ‘Ninja’ ambaye jana Jumatano anarejea nchini akitokea Tunisia alikokwenda kufanyiwa upasuaji wa mguu wa kushoto.

Kichapo cha bao 1-0, walichopata Simba juzi Jumatatu dhidi ya Mbeya City, kimemfanya Ninja apate furaha, kisha kuwaambia wangeongeza na droo mchezo unaofuata itawapa nafasi wao kujiimarisha kileleni.

Yanga ndio kinara wa pointi 32, inamiliki mabao 22 na imefungwa mabao manne baada ya kucheza mechi 12, kushinda 10 na kutoka sare mbili dhidi ya Namungo na Simba.

Jambo lililompa kicheko Ninja baada ya kuona watani wao wa jadi Simba, wanawapiga gepu kubwa la pointi (8).

“Kiukweli nawapongeza Simba kwa muenendo wao, ingekuwa vizuri zaidi mechi inayofuata wangetoka sare ili kuendelea kutupa kicheko,”amesema Ninja na ameongeza kuwa;

“Kuna vitu vinavyoweza kumpa furaha mgonjwa jamani, nimejikuta nijisikia vizuri baada ya kupata matokeo ya mkoani Mbeya ya jana,”amesema.

SOMA NA HII  KUELEKEA DIRISHA DOGO...KISINDA 'OUT' MBRAZILI WA SINGIDA 'IN'...ISHU NZIMA IKO HIVI..