Home Habari za michezo KUELEKEA DIRISHA DOGO…KISINDA ‘OUT’ MBRAZILI WA SINGIDA ‘IN’…ISHU NZIMA IKO HIVI..

KUELEKEA DIRISHA DOGO…KISINDA ‘OUT’ MBRAZILI WA SINGIDA ‘IN’…ISHU NZIMA IKO HIVI..

Yanga inaona bado inakosa huduma ya winga wa kisasa anayejua kutengeneza mashambulizi makali wakati wakisubiri ratiba ya kujua wataangukia kundi lipi katika hatua ya Makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika lakini kuna mtu wanampigia hesabu ndefu.

Yanga bado wanapiga hesabu waingie vipi Singida Big Stars kupata saini ya winga wa Kibrazil Dario Frederico ambaye amendelea kuwa na mwanzo mzuri katika ligi.

Yanga inaona kuwa Dario ana ufundi mwingoi ambao unaweza kuwasaidia baada ya Mkongomani Tuisila Kisinda kuanza vibaya katika kikosi hicho tangu arejee kwa mkopo.

Mabosi wa Yanga wanafikiria kama Kisinda ataendelea kuwa na kiwango cha kusua sua huenda akarudishwa katika klabu yake ya RS Berkane ambapo wataendelea kumfuatilia mpaka kipindi cha dirisha dogo.

Dario ndiye winga anayepewa nafasi kubwa ya kuchukua jezi ya Kisinda kuja kuiongezea nguvu Yanga endapo mabosi wa Singida wakilainika kumuachia.

Yanga itaanza kupigania heshima yao katika hatua ya makundi Februari mwakani ambapo ratiba ya makundi itakapotoka Novemba 16 wiki ijayo.

Mapema tu Yanga iligundua ubora wa winga huyo na kujaribu kutaka kumsajili hata kabla ya dirisha dogo kufungwa lakini inaelezwa kocha wa Singida Mdachi Hans Pluijm alizuia jaribio hilo akiwaeleza mabosi wake kwamba bado anamtaka winga huyo asalie hapo.

SOMA NA HII  HILI HAPA JESHI KAMILI LA SIMBA 2021/22