Home news WAKATI SIMBA WAKIPANGA KUSHUSHA ‘FULL’ KIKOSI LEO…KOCHA WA SALLEM VIEW ‘ALIA MAPEMA’..

WAKATI SIMBA WAKIPANGA KUSHUSHA ‘FULL’ KIKOSI LEO…KOCHA WA SALLEM VIEW ‘ALIA MAPEMA’..

 


KUNA balaa Zenji raundi hii. Simba imepeleka mziki kamili katika Kombe la Mapinduzi kuthibitisha wanalitaka taji hilo ambalo wanaanza kulisaka leo katika mechi yao ya kwanza dhidi ya Sallem View ya Zanzibar itakayopigwa kuanzia saa 10 jioni.

Mashabiki wa timu hiyo ambayo katika mechi iliyopita iliipelea puta Azam ikimiliki mpira hadi asilimia 80 kwa 20 za wanalambalamba, wametamba kuwa watu waje hapa kisiwani kuhesabu mabao tu kuanzia leo.

Ni nyota wawili tu, Taddeo Lwanga na Erasto Nyoni watakaoendelea kukosekana kutokana na majeraha.

Lakini wakati hao wakikosekana tayari kuna nyota wawili wapya ambao walianza mazoezi yao ya majaribio ya kuwania kusajiliwa na kuamsha mizuka ambao ni winga wa kushoto kutoka Ivory Coast, Moukoro Cheik (30), na kiungo wa zamani wa klabu hiyo ya Msimbazi, Sharaf Eldin Shiboub na hivyo kufanya kikosi kuwa imara zaidi.

Habari zaidi zinaeleza kuwa huenda nyota wengine wakaendelea kuongezeka ndani ya kikosi cja Simba hasa wakati huu wa usajili wakiyatumia mashindano hayo ambayo nayatarajia kumalizika Januari 13 mwaka huu.

Simba ilifanya mazoezi yao ya kwanza juzi na jana jioni walimalizia mazoezi yao ya mwisho kuelekea mechi hiyo itakayochezwa Uwanja wa Amaan kisiwani hapa.

Wakati Simba wakitamba kushinda mechi hiyo na nyingine ili kubeba kombe wapinzani wao ambao nao wametamba kuondoka na pointi tatu baada ya kubanwa kwa sare 0-0 dhidi ya Mlandege katika mechi yao ya ufunguzi juzi.

Mchezaji wa Simba Gadiel Michael alisema wamejipanga kupambana kuhakikidha wanaanza vizuri kwani wanalitaka kombe hilo ambalo walilipoteza msimu uliopita.

“Tumejiandaa vizuri na tunataka kuwa na mwanzo mzuri kwenye mashindano haya. Tunafahamu kuwa Wazanzibari wanalitaka hili kombe lakini hata sisi tunataka kulichukua hivyo mchezo hautakuwa rahisi na hatutawadharau wapinzani wetu,” alisema Gadiel.

Naye Meneja wa timu hiyo, Patrick Rweyemamu aliwazungumzia wachezaji walioanza mazoezi.

“Kuna wachezaji wawili wapya wameanza mazoezi jana (juzi) na huenda mtaendelea kuwaona wapya wengine ama lah ila kikosi kipo imara na tunawaheshimu wapinzani wetu. Dakika 90 ndizo zitakazoamua maana huu ni mpira unachezwa uwanjani.

SOMA NA HII  A-Z JINSI GEITA GOLD WALIVYOWANYANYASA SIMBA KWENYE UWANJA WA CCM KIRUMBA...PABLO ALIFANYA YOTEE...

“Leo (jana)jioni tutafanya mazoezi ya mwisho hivyo tumejipanga kwa kweli katika kuusaka ubingwa wa michuano hii,” alisema Rwenyemamu

Naye kocha mkuu wa Sellem View, Ali Omari alisema kuwa ushindi ni lazima; “ni mechi ngumu kwa pande zote mbili mbaya zaidi tulipoteza mechi ya kwanza hatuwezi kukubali kupoteza ya pili, nimewajenga kisaikolojia wachezaji wangu ili wasiwahofie nyota wa Simba,”

Kocha huyo alisema mbali na kuwajenga nyota wake kisaikolojia lakini anafahamua udhaifu wa Simba ulipo na amewapa maelekezo wachezaji wake.

“Tukifungwa na Simba haitakuwa habari kwetu na kitakuwa ni kitu cha kawaida ila tukitoka sare ama kushinda basi tutakuwa tumepiga hatua kubwa sana na itakuwa ni historia. Nimewaelekeza wachezaji wangu kuwa wakifanya makosa mengi basi tutafungwa mabao mengi, yakiwa makosa machache na idadi itakuwa ndogo na kama hakutakuwa na makosa basi hatutafungwa.

“Simba ni timu kubwa na ina wachezaji wakubwa lazima tuwaheshimu wametuzidi kwa kila kitu ila hatutaki kuogopa ukubwa wa màjina ya wachezaji wao tutapambana tuwezavyo,” alisema Omari.