Azam FC

BAADA YA KUANZA KUSHINDA-SHINDA MECHI ZAO…AZAM FC WATOA MKWARA WA KUFA MTU..ZAKA ZAKAZI ANENA HAYA..

admin February 6, 2022 8:18 am


UONGOZI wa Azam FC umeweka wazi kuwa malengo yao makubwa msimu huu ni kuhakikisha wanashinda michezo mingi kadiri inavyowezekana ili kujiweka kwenye nafasi nzuri katika msimamo na kukata tiketi ya kucheza mashindano ya kimataifa msimu ujao.

Azam ambayo ipo chini ya kocha Abdi Hamid Moallin, kabla ya michezo ya jana ilikuwa kwenye nafasi ya nne na pointi zao 21 walizokusanya kwenye michezo 13.

Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Azam, Zakaria Thabith ‘Zaka Zakazi’ amesema  kuwa: “Tunajua wazi kuwa ligi ya msimu huu ni ngumu na kama klabu kila mtu anajua ni namna gani tulipitia kipindi kigumu mwanzoni mwa msimu huu, lakini kwa sasa tumerekebisha sehemu kubwa ya mapungufu tuliyokuwa nayo.

“Malengo yetu makubwa ni kuhakikisha tunashinda michezo yetu ijayo kadiri itakavyowezekana ili kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kushiriki mashindano ya Afrika msimu ujao.”

KILICHOMPONZA MORRISONI HIKI HAPA…ISHU YA BOCCO , CHAMA KUMBE IKO HIVI…SHABIKI ASIYEONA AIBUA MAPYA.. BAADA YA YANGA KUTELEZA JANA…PABLO FASTA AIBUKA NA MBINU HII..AFUNGUKA JINSI ‘ATAKAVYOKULA VICHWA’..

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply