News

PAMOJA NA KUSHINDA MECHI..MASTAA SIMBA WACHIMBWA MKWARA…MATOLA AMNYOOSHEA KIDOLE BOCCO..

admin February 8, 2022 3:22 pm


KOCHA Msaidizi wa Simba, Seleman Matola, amefunguka kuwa benchi la ufundi la klabu hiyo halijaridhishwa na mwenendo wa ufungaji mabao ndani ya kikosi chao na tayari wamekaa na mastraika wa kikosi hicho kuangalia namna ya kumaliza tatizo hilo.

Simba msimu huu wamekuwa na changamoto kubwa kwenye safu ya ushambuliaji ya timu hiyo ambapo kabla ya mchezo wa jana walikuwa wamefanikiwa kufunga mabao 15 tu, katika michezo yao 14 ya mzunguko wa kwanza waliyokuwa wamecheza.

Kwenye Ligi Kuu Bara mpaka sasa kwa Simba ni Meddie Kagere pekee ambaye amefanikiwa kuandikisha mabao msimu huu akiwa tayari amefunga mabao matano, huku John Bocco na Chris Mugalu wao wakiendelea kuwa na ukame wa mabao.

Akizungumzia changamoto ya safu yao ya ushambuliaji msimu huu, kocha Matola alisema: “Kama benchi la ufundi tunakiri kuwa ni kweli tumekuwa na changamoto katika safu yetu ya ushambuliaji msimu huu, tatizo ambalo kama benchi la ufundi tunalifanyia kazi ili kuhakikisha linamalizika na tunafunga mabao.

“Tayari tumekaa na washambuliaji wetu na kuangalia wapi tunakosea ili kurekebisha, pia kuwaweka wazi kuwa hatuhitaji kuona hali hii inaendelea.”

WAKATI WADAU WAKIWA WANALIA KUSHUKA KWA VIWANGO VYA CHAMA NA BOCCO…DANTE AIBUKA NA HILI JIPYA.. BAADA YA KUKINUKISHA SIMBA…MGHANA WA AZAM AMPA SOMO MORRISON…AFUNGUKA YASIRINI…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply