news

WAKATI WADAU WAKIWA WANALIA KUSHUKA KWA VIWANGO VYA CHAMA NA BOCCO…DANTE AIBUKA NA HILI JIPYA..

admin February 8, 2022 11:55 am


MASTAA wa zamani Yanga, Andrew Vicent ‘Dante’ na Farouk Shikhalo kwa nyakati tofauti wamewasifu nyota wa Simba, Clatous Chama na John Bocco kuwa bado wapo kwenye viwango vizuri licha ya kuonekana kutokuwa kwenye kasi yao iliyozoeleka.

Bocco hadi sasa hajaonyesha makali yake huku akiwa hajafunga bao lolote wakati upande wa Chama naye anaonekana hajachanganya tangu alivyorejea kikosini hapo.

Dante akimzungumzia Bocco alisema anashangazwa na mashabiki wakimbeza mshambuliaji huyo kwani suala la kufunga ni la muda na linaweza kumtokea mchezaji yeyote.

Alisema hata yeye wakati wa dabi alipokuwa akiichezea Yanga na hata msimu uliopita (KMC) walipokutana na Simba alikuwa anajua anaenda kukutana na ugumu.

“Bocco ni mchezaji mwenye kasi kubwa anapokuwa uwanjani, ukikimbizana naye kwenye kuwania mpira inabidi ujipange kwa sababu ana nguvu na bado anajua kufunga,” alisema Dante.

Kwa upande wa Shikhalo alisema suala la Chama watu kumchukulia wa kawaida wanakosea kwani kushindwa kuonyesha kitu kikubwa inatokana na changamoto anazopitia. “Atakuwa sawa na watu watanyamaza, inawezekana alipokuwa hakupata muda mwingi wa kucheza na ndio maana imekuwa hivi lakini kwangu atabaki kuwa bora siku zote,” alisema.

Simba ilimuuza Chama timu ya RS Berkane mwaka jana, lakini amerejea Msimbazi.

USHINDI WA SIMBA DHIDI YA MBEYA KWANZA WAMUIBUA MASAU BWIRE…ADAI SOKA HALINA MWENYEWE… PAMOJA NA KUSHINDA MECHI..MASTAA SIMBA WACHIMBWA MKWARA…MATOLA AMNYOOSHEA KIDOLE BOCCO..

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply