news

BODI YA LIGI WAVUNJA UKIMYA ISHU YAO NA GSM…WAFUNGUKA MADUDU ZAIDI YA MKATABA WA UDHAMINI…

admin February 11, 2022 4:00 am


MWENYEKITI wa Bodi ya Ligi Kuu Bara, Steven Mnguto, ameibuka na kusema licha ya wadhamini wenza Kampuni ya GSM kutangaza kujiondoa katika udhamini lakini hakuna klabu yoyote iliyolipwa.

Kauli hiyo imekuja ikiwa ni siku moja tangu GSM watangaze kujiondoa kudhamini klabu za ligi ambazo awali waliingia mkataba wa miaka miwili wenye thamani ya Sh 2.1Bil.

Akizungumza na gazeti la Championi Jumatano, Mnguto alisema kuwa, hilo suala wamepanga kulizungumza hivi karibuni mara baada ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) watakapokutana.

Mnguto alisema kuwa, wanasubiria wanasheria wao walipitie suala hilo na mwisho wa siku watalitolea ufafanuzi kwa undani.

“Kiukweli tangu tuliposaini mkataba na GSM nikiri klabu hazijapata chochote. Klabu zimeitangaza GSM kwa muda wa miezi mitatu sasa, kwa hiyo tunasubiri wanasheria walipitie suala hilo tujue tunafanyaje.

“Hata suala la zile nembo kwenye mabega sijui kama zinaweza kutolewa haraka lakini hata hilo litafanyiwa kazi kisheria,” alisema Mnguto.

Naye Mkurugenzi wa Habari na Masoko wa TFF, Boniface Wambura, akizungumzia hilo alisema: “Sisi baada ya kupata barua kutoka GSM, suala la mkataba ni Bodi ya Ligi na ni vema akatafutwa Mnguto lakini kwa upande wa sisi TFF hatuwezi kuzungumzia kila jambo.

“Tayari tumetoa tamko letu jana (juzi) kuhusiana na hilo baada ya kupata barua GSM.” Juzi TFF ilitoa taarifa kuwa, Februari 7, mwaka huu walipokea barua ya kuvunja mkataba wa udhamini mwenza wa Ligi Kuu Bara ya NBC kutoka Kampuni ya GSM, hivyo Shirikisho hilo linafanyia kazi barua hiyo na litatoa taarifa kwa wadau.

MO AFANYA KUFRU NYINGINE SIMBA…ATOA KAULI YA MWAKA KUELEKEA MECHI NA WAIVORY…SASA NI MSELELEKO TU… KISA PRESS YA MANARA NA MWENZAKE…AZAM WASHINDWA KUKAA KIMYA…WAJIBU NAMNA ‘WANAVYOPIGWA’ KWENYE LIGI…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply