Home news BAADA YA KUONA VIWANGO VYA MAKIPA YANGA…MBRAZILI AGUNA KISHA AKATOA HILI..ADAI ITAKUWA...

BAADA YA KUONA VIWANGO VYA MAKIPA YANGA…MBRAZILI AGUNA KISHA AKATOA HILI..ADAI ITAKUWA NGUMU…


KOCHA wa Makipa wa Yanga, Mikton Nienov amewasifu makipa wake, Djigui Diarra, Aboutwaleb Mshery na Erick Johora wotw kwa pamoja wanafanya vizuri na kuisaidia timu yao.

“Namshukuru Mungu kwa timu yetu kuwa na walinda milango mahiri ambao hawajapishana sana viwango vyao. Kazi yetu benchi la ufundi, ni kuboresha viwango vyao, kuvikuza, kulinda na kuweka ushindani ndaji yao ili kuleta matokeo chanya kati yao na timu kwa ujumla.

“Tupo katika FA na ligi kuu na malengo ya klabu ni kufanya vyema kwenye ligi zote, hivyo ni lazima kumsaidia kocha mkuu kuandaa wachezaji wote katika ubora mzuri ili awe na uwanja mpana wa kuwatumia.

“Kuna injury, national call ups, cards, matatizo binafsi, kushuka kiwango, hivyo kama hutakuwa na wachezaji wazuri wenye kuendana viwango kila idara, itakuwa ngumu kushindana na wenzako wenye depth kubwa kwenye selection ya wachezaji,” amesema Milton.

SOMA NA HII  SAA KADHAA KABLA YA KUSHUKA DIMBANI HUKO NIGER..BOCCO AIBUKA NA HILI JIPYA...AOMBA DUA...