Home news A-Z JINSI YANGA WALIVYOKULA MIWA YA MTIBWA…MAYELE AKOLEZA MOTO..AKABIDHIWA NG’OMBE…

A-Z JINSI YANGA WALIVYOKULA MIWA YA MTIBWA…MAYELE AKOLEZA MOTO..AKABIDHIWA NG’OMBE…


USHINDI wa mabao 2-0 waliopata Yanga dhidi ya Mtibwa Sugar unaifanya timu hiyo kuendeleza rekodi yake ya mwisho ya ushindi katika uwanja wa Manungu.

Yanga mara ya mwisho kucheza katika huo ni Mwaka 1992 huku wakipata ushindi wa mabao 4-2.

Katika mchezo huo Yanga ndio walikuwa wa kwanza kupata bao la kuongoza katika dakika 45 za kipindi cha kwanza kupitia kwa Ntibazonkiza n kuwafanya waende mapumziko wakiongoza.

Kipindi cha pili Mtibwa walianza kwa kufanya mabadiliko ya kumtoa Salum Kihimbwa na kuingia Nassor Kiziwa.

Mpira ulizuka utata dakika 48 Feisal alipoiifungia Yanga bao akiunganisha krosi ya Djuma, bao hilo lilikataliwa na mwamuzi akisema lilifungwa kwa mkono.

Mwamuzi wa mchezo huo alilazimika kufuta bao hilo na kumfuata Feisal Salum na kumuonyeshea kadi ya njano.

Dakika 56 mshambuliaji wa Mtibwa Sugar, George Makang’a alionyeshewa kadi ya njano baada ya kumfanyia madhambi nahodha wa Yanga, Bakari Mwamnyeto.

Mtibwa walifanya mabadiliko ya kuwatoa Said Ndemla na Makang’a huku nafasi zao wakiigia Jafar Kibaya na Ismail Mhesa.

Mabadiliko ya Mtibwa yalionekana yanaenda kuongeza nguvu kwenye eneo la ushambuliaji.

Dakika 62 Mayele alipata nafasi ya kufunga bao la pili baada ya kuingia na mpira ndani ya boksi lakini beki wa Mtibwa, Ame Ally akimkatalia kwa kuokoa shambulizi hilo.

Baada ya tukio hilo Ame alionyesha kuumia na madaktari wa timu hiyo walimfanyia matibabu na kupooza maumivu yake.

Dakika 67 Yanga ilipata bao la pili baada ya Sure Boy kupiga pasi kwa Ntibazonkiza na yeye alimrudishia  na Sure alipenyeza pasi nyingine kwa Ntibazonkiza ambaye alipiga pasi kwa Mayele aliyewekwa mpira huo wavuni.

Wahezaji wa Yanga, Fiston Mayele akishangilia bao lake baada kupokea pasi kutoka kwa Saido Ntibazonkiza.

Mtibwa Sugar walifanya shambulizi kupitia kulia baada ya Ismail Mhesa kupiga krosi na Jafar Kibaya alipiga shuti na kutoka nje ya goli.

Dakika 69 Mtibwa walimtoa Ibrahim Ame na nafasi yake aliingia Dickson Daud wakati huo huo Yanga walifanya mabadiliko dakika 72 wakiwatoa Denis Nkane na Salum Abubakary ‘Sure Boy’ na kuingia Deus Kaseke na Zawadi Mauya.

SOMA NA HII  ANAYEFUATA KUTAMBULISHWA SIMBA HUYU HAPA....TAYARI YUKO ZAKE ZNZ MAPEMA TU...

Dakika 75 Mtibwa Sugar walifanya mabadiliko mengine ya kumtoa Brian Mayanja na kuingia Boban Zirintusa.

Mabadiliko ya kuingia Mhesa kwenye kikosi cha Mtibwa yalionekana kuwa na tija baada ya mchezaji huyo kuwa na wepesi kwenye kupeleka mashambulizi.

Upande wa Kibaya mara kwa mara alipokuwa anapokea mpira alikuwa anageukia golini kwao na kuwafanya mabeki wa Mtibwa wasipate tabu ya kumkaba.

Dakika 79 Yanga walifanya mabadiliko ya kumtoa Mayele na nafasi yake aliingia Heritier Makambo.

Mshambuliaji huyo dakika 80 alipata nafasi ya kuwanyanyua mashabiki wa Yanga baada ya kupokea pasi ya Ntibazonkiza nje kidogo ya boksi lakini shuti lake halikulenga lango.

Dakika 83 Yanga walifanya mabadiliko mengine ya kumtoa Ntibazonkiza na nafasi yake aliingia Dickson Ambundo.

Ndani ya dakika moja (Dakika 84) Ambundo naye alipata nafasi ya kuifungia Yanga bao la tatu baada ya kumtoa beki wa Mtibwa lakini alipoingia ndani ya boksi utulivu alikosa na kupiga shuti lililopaa juu ya goli.

Mara baada ya mchezo huo, Shabiki wa Yanga mkoni Mororgoro, alijitokeza mbele ya uongozi wa Yanga na kutoa ahadi ya zawadi ya Ng’ombe dume kwa mshambuliaji kinara wa Yanga, Mayele.

Aidha, kocha wa Yanga Nabi naye ametunukiwa zawadi kama hiyo kutoka kwa shabiki huyo.