Home CAF BAADA YA KUIONA SIMBA INAVYOCHEZA…KISINDA KAKUNA KICHWAA WEE..KISHA AKASEMA HAYA..

BAADA YA KUIONA SIMBA INAVYOCHEZA…KISINDA KAKUNA KICHWAA WEE..KISHA AKASEMA HAYA..


YULE winga wa zamani wa Yanga kwenye kasi ya kishada, Tuisila Kisinda ambaye sasa anaitumikia RS Berkane, ameipiga mkwara Simba akidai hasira ya kipigo walichopewa na Asec Mimosas zitaishia kwao wakati timu hizo zitakapokutana katika mechi itakayopigwa Jumapili hii.

Simba na Berkane zipo Kundi D la michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika na Jumapili usiku zitavaana, kila mmoja ikiwa na kiu ya ushindi baada ya Wamorocco hao kulazwa 3-1 ugenini na Asec, huku Simba ikitoka sare ya 1-1 dhidi ya USGN.

Akizungumza kutoka Morocco, Kisinda alisema matokeo yaliyopita yalikuwa ni bahati mbaya kwao na sasa wanarudi nyumbani kujipanga ili kushinda dhidi ya Simba na kujiweka pazuri kwenye msimamo wa kundi hilo.

“Simba nawajua ni wazuri na matokeo waliyoyapata ugenini yamewapa nguvu, lakini nasi tumejipanga na tunataka tu ushindi dhidi yao bila kuangalia idadi ya mabao,” alisema Kisinda ambaye kasi yake iliwasumbua sana mabeki wakiwamo wa Simba katika Kariakoo Derby.

Hata hivyo, Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez na Kocha Pablo Franco walisema jana wakiwa Morocco kwamba wameenda nchini humo ili kupata ushindi kwani malengo yao kufika mbali anga za kimataifa.

SOMA NA HII  KUHUSU UWANJA WA SIMBA...MAMBO YAANZA HUKOOO...BARBARA ATINGA 'SITE' NA WATAALAMU...KUANZA NA MAJUKWAA...