Home news BAADA YA KUKINUKISHA SIMBA…MGHANA WA AZAM AMPA SOMO MORRISON…AFUNGUKA YASIRINI…

BAADA YA KUKINUKISHA SIMBA…MGHANA WA AZAM AMPA SOMO MORRISON…AFUNGUKA YASIRINI…


KUTOKANA na winga wa Simba, Bernard Morrison kupewa adhabu ya utovu wa nidhamu, Mghana mwenzake wa Azam, Daniel Amoah, amempa somo.

Wawili hao ambao ni marafiki na wametoka kijiji kimoja, wamekuwa wakikutana mara kwa mara na kushauriana. Morrison ameadhibiwa na Simba kwa kosa la kinidhamu la kutoroka kambini na alipoambiwa asirudi mpaka atakapoongea na mtendaji mkuu pia alikaidi. Winga huyu wa Simba ambaye aliwahi kuichezea Yanga, pia alikuwa na matukio ya namna hiyo akiwa Yanga.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Amoah amesema: “Huwa naongea na Morrison mambo mengi sana na tunashauriana, namuombea aweze kupatana na timu yake na kuweza kurejea kambini. “Ni mchezaji mzuri na hata kwa hili la kusimamishwa tumeongea, nina imani watakuwa sawa,” alisema Amoah.

SOMA NA HII  KOCHA SIMBA ATAJA SABABU YA BOCCO KUWA MFUNGAJI BORA