Home Simba SC KOCHA SIMBA ATAJA SABABU YA BOCCO KUWA MFUNGAJI BORA

KOCHA SIMBA ATAJA SABABU YA BOCCO KUWA MFUNGAJI BORA


 DIDIER Gomes, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa anaamini kwamba tuzo ya mfungaji bora itakuwa mikononi mwa washambuliaji wake wanaoongozwa na nahodha John Bocco mwenye mabao 15 kutokana na juhudi walizonazo.


Tuzo hiyo kwa sasa ipo mikononi mwa Meddie Kagere mwenye mabao 11 huku ushindani ukizidi kukomelewa na Prince Dube wa Azam FC mwenye mabao 14, Chris Mugalu mwenye mabao 13 na Luis Miquissone mwenye mabao tisa wote wanakipiga ndani ya Simba

Wengine ni Danny Lyanga wa JKT Tanzania, Meshack Abraham wa Gwambina, Idd Seleman wa Azam FC, Yusuph Mhilu wa Kagera Sugar hawa wana mabao 9 huku Yacouba Songne wa Yanga akiwa na mabao 8.

Akizungumza na Spoti Xtra, Gomes alisema kuwa washambuliaji wake wote wakiongozwa na Bocco wanaonekana kuwa na uhitaji wa kufunga mabao mengi jambo ambalo anaamini litawapa tuzo.

“Hawachezi kwa ajili ya tuzo lakini wapo tayari kufunga kuanzia Bocco, (John), Kagere na Mugalu wote napenda kazi yao wakiwa uwanjani, kwa namna ambavyo wanapambana ni wazi kwamba watapata tuzo ya ufungaji bora.

“Ushindani kutoka sehemu nyingine upo kwani ukitazama wachezaji wa Azam FC wanafanya vizuri na hata tukikutana na timu nyingine zinafanya vizuri, kikubwa ni suala la kusubiri na kuona, kila kitu kinawezekana,” alisema Gomes.

SOMA NA HII  KUYEYUKA KWA DABI, HAJI MANARA AOMBA MSAMAHA