Home Simba SC SIMBA KUSEPA DUBAI LEO KUWAFUATA AL AHLY MISRI

SIMBA KUSEPA DUBAI LEO KUWAFUATA AL AHLY MISRI


WAWAKILISHI wa Tanzania kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, Simba leo Aprili 7 wanatarajiwa kuanza safari kuelekea Misri, baada ya jana Aprili 6 kuweka mapumziko Dubai.

Simba ilisepa na msafara wenye watu 55 ikiwa ni pamoja na wachezaji, benchi la ufundi pamoja na viongozi.

Kitaanza kuwafuata wapinzani wao Al Ahly kwa ajili ya kumaliza mchezo wao wa mwisho wa hatua ya makundi.

Kwenye msimamo Simba ipo nafasi ya kwanza katika kundi A baada ya kukusanya pointi 13 inakutana na Al Ahly ambayo ipo nafasi ya pili na pointi zake kibindoni ni 8.

Timu hizi mbili zimefuzu hatua ya robo fainali huku AS Vita iliyo nafasi ya tatu na pointi nne pamoja na Al Merrikh iliyo nafasi ya nne na pointi 2 ikikwama kutinga hatua ya robo fainali kwenye hatua ya makundi.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Aprili 9, nchini Misri ambapo Al hly wanakumbuka kwamba walipotua Bongo, walipotezwa kwa kufungwa bao 1-0 lililopachikwa na Luis Miquissone kwa pasi ya Clatous Chama na wote wapo kwenye msafara.

Wengine ambao wapo kwenye msafara wa Simba kwa upande wa wachezaji ni pamoja na Meddie Kagere, Bernard Morrison, Said Ndemla, Ibrahim Ajibu, John Bocco na Rarry Bwalya.

Kwa upande wa viongozi ni Ofisa Habari Haji Manara, Mtendaji Mkuu, Barbara Gonzalez.

Meneja wa Simba, Patrick Rweyemamu amesema kuwa wanakwenda kushindana na wanaamini watapata matokeo chanya.

SOMA NA HII  PABLO NA CHAMA WAIKUNG'UTA YANGA TUZO ZA MWEZI MACHI...NABI 'ATIMULIWA VUMBI JEUSI'...