Home Ligi Kuu BIASHARA UNITED INAMSAKA MRITHI WA MIKOBA YA BARAZA

BIASHARA UNITED INAMSAKA MRITHI WA MIKOBA YA BARAZA


 SELEMAN Mataso, Mwenyekiti wa Klabu ya Biashara United amesema kuwa mchakato wa kumsaka mrithi wa mikoba ya Francis Baraza bado unaendelea.

Baraza alikuwa na Biashara United ambapo alikiongoza kikosi hicho kwenye mechi 23 na kipo nafasi ya nne baada ya kukusanya pointi 39 katika ligi.

Kwa sasa Baraza ni Kocha Mkuu wa Klabu ya Kagera Sugar iliyoachana na kocha wao Mecky Maxime kwa kile walichoeleza kuwa mwendo mbovu wa timu hiyo.

Maxime alikiongoza kikosi hicho kwenye mechi 24 na kipo nafasi ya 13 pointi zake ni 25.

Mataso amesema kuwa bado kazi inaendelea ya kumsaka kocha mpya ikikamilika atatangazwa.

“Mchakato wa kumsaka kocha mpya unaendelea na unahitaji umakini kwa sababu kocha yeye anakuwa na jukumu la kuongoza kikosi kupata ushindi.

“Unaona kwamba tumekuwa kwenye mwendo mzuri kwa msimu huu hivyo tunahitaji kuendelea kubaki kwenye mfumo na mwalimu ambaye atakuja ni lazima aweze kwenda na kasi ambayo tupo nayo,” amesema.

SOMA NA HII  BIASHARA UNITED YAKOMALIA TANO BORA