Home Habari za michezo PABLO NA CHAMA WAIKUNG’UTA YANGA TUZO ZA MWEZI MACHI…NABI ‘ATIMULIWA VUMBI JEUSI’…

PABLO NA CHAMA WAIKUNG’UTA YANGA TUZO ZA MWEZI MACHI…NABI ‘ATIMULIWA VUMBI JEUSI’…


Kiungo wa Simba Clatous Chota Chama amefanikiwa kuibuka mchezaji bora wa mwezi Machi Ligi Kuu Tanzania Bara, NBC Primia Ligi.

Wakati Chama akiibuka mchezaji Bora, Kocha wa Simba Pablo Franco Martin amechaguliwa kuwa Kocha Bora wa Mwezi Machi Ligi Kuu Bara.

Chama ameibuka kidedea akiwapiku Fiston Mayele wa Yanga na Frank Kahole wa Mtibwa Sugar.

Kwa mwezi Machi, Chama amecheza michezo miwili na kufunga magoli mawili huku michezo yote miwili wakiibuka na ushindi.

Kwa Upande wa Kocha Pablo amewagaragaza Nasreddine Nabi wa Yanga na Francis Baraza wa Kagera Sugar baada ya kufanikiwa kuingoza Simba kushinda michezo yake miwili dhidi ya Biashara United na Dodoma Jiji.

Mbali na hao tuzo ya Meneja Bora wa Uwanja imekwenda kwa Gordon Nsajigwa, Meneja wa Uwanja wa Benjamin Mkapa.

SOMA NA HII  WAKATI SIMBA WAKITAMBA NA BEKI WAO MCAMEROON...YANGA WAMESHUSHA CHUMA HIKI CHA KAZI...