Home news BAADA YA TETESI ZA SIMBA KUMNYATIA MWAMNYETO KUWA NYINGI…YANGA FASTA WAIBUKA NA...

BAADA YA TETESI ZA SIMBA KUMNYATIA MWAMNYETO KUWA NYINGI…YANGA FASTA WAIBUKA NA HILI JIPYA…


UONGOZI wa Yanga, umezima tetesi za kuondokewa na baadhi ya wachezaji wake ambao mikataba yao inatarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu kwa kusema hao wanaowahitaji wanajisumbua na badala yake mastaa hao wataendelea kukipiga Jangwani.

Baadhi ya wachezaji wa Yanga ambao mikataba yao inatarajiwa kumalizika mwisho wa msimu huu ni nahodha Bakari Mwamnyeto anayetajwa kuwaniwa na Simba.

Wengine ni Dickson Job, Kibwana Shomari, Saidi Ntibazonkiza ‘Saido’, Yacouba Songne, Deus Kaseke na Abdallah Shaibu ‘Ninja’ ambaye hivi karibuni alipelekwa nchini Tunisia kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji wa goti.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo zimepatikana, kutoka kwa mmoja wa mabosi wenye ushawishi ndani ya timu hiyo, alisema wachezaji hao wameshamaliza mazungumzo ya awali kwa ajili ya kuongeza mikataba kuendelea kukipiga Yanga.

Bosi huyo alisema kabla ya kuanza mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara, baadhi ya wachezaji hao watakuwa wamesaini mkataba baada ya kukamilishiwa mahitaji yao muhimu ikiwemo mshahara.

Aliongeza kuwa, ni ngumu kwa uongozi wa timu hiyo kukubali kuwaachia kirahisi wachezaji hao akiwemo Mwamnyeto, Job, Kibwana na Saido ambao wapo kikosi cha kwanza.

“Mashabiki waondoe hofu juu ya wachezaji wetu hao kwenda Simba, kati ya hao wanaotajwa wote wameonesha nia na kukubali kuendelea kubaki Yanga.

“Hivyo Mwamnyeto hatakwenda popote, waacheni waendelee kujidanganya hao wanaotangaza kutaka kumsajili,” alisema bosi huyo.

Mkurugenzi Uwekezaji wa GSM ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya Mashindano ya Yanga, Injinia Hersi Said, aliwahi kusema  kuwa: “Hizo zinazoendelea ni tetesi tu, achana nazo hakuna mchezaji yeyote tunayemuhitaji tutakayekubali kumuachia akiwemo Shomari na Mwamnyeto.”

Naye Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Frederick Mwakalebela, alisema: “Hao wanaotangaza kumsajili Mwamnyeto wameshakata tamaa ya ubingwa wa ligi, hivi sasa wamehamia katika propaganda. Hakuna mchezaji tunayemuhitaji tukamuachia akaondoka.”

SOMA NA HII  FEISAL SALUM LEO MKWAWANI KUNACHIMBIKA , YANGA WAJIPANGE